↧
VIDEO: Jionee Wema Sepetu akicheza vigoma Tanga
↧
TANZIA: Samwel Sitta Afariki Dunia
↧
↧
Rayvanny - SUGU (Official Video Music)
↧
Benki ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) itaanza kutoa baadhi ya huduma za kibenki Novemba 8, 2016.
Kwa mamlaka iliyopewa kisheria kupitia kifungu namba 58(2) (a) na (b) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu inapenda kuutarifu umma kwamba zoezi la tathmini ya hali ya kifedha ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) limekamilika; kwa mantiki hiyo, Twiga itaanza kutoa baadhi ya huduma za kibenki kwa umma kuanzia Jumanne tarehe 8 Novemba 2016.
Huduma hizo ni pamoja na ukusanyaji wa marejesho ya mikopo ya wateja. Meneja Msimamizi wa benki hiyo atawajulisha wateja huduma zitakazotolewa na taratibu za kuzingatia.
Benki Kuu ipo katika mchakato wa kupitia na kuchambua njia mbadala za kutatua tatizo la mtaji linaloikabili Twiga Bancorp. Njia inayopewa kipaumbele ni kutafuta mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya, mchakato utakaowahitaji kuchambua hali halisi ya taarifa za hesabu za Twiga (due diligence).
Zoezi hili linatarajiwa kuchukua takribani wiki tatu na litakapokamilika, Benki Kuu itaingia makubaliano na wawekezaji wapya kuhakikisha wanaingiza mtaji unaohitajika haraka iwezekanavyo ili shughuli za kawaida za kibenki ziweze kuendelea.
Benki ya Twiga itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu hadi hapo utaratibu wa kuwamilikisha wawekezaji wapya utakapokamilika.
Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuiweka Twiga Bancorp Ltd chini ya usimamizi wake kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016 kutoka na upungufu mkubwa wa mtaji unaoikabili.
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.
BENKI KUU YA TANZANIA
6 Novemba, 2016
↧
Afrima Awards: Diamond Platnumz aondoka na tuzo tatu (Picha/Video)
Diamond Platnumz ameibuka na ushindi wa nguvu kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria. Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa.

Diamond akishukuru baada ya kushinda tuzo ya tatu kwenye Afrima
Pamoja na ushindi huo, Diamond pia alitumbuiza wimbo alioimba na Papa Wemba, msanii aliyetunukiwa tuzo ya heshima.
Wasanii wengine waliotumbuiza ni pamoja na Patoranking, P-Square, Falz, Eddy Kenzo, Avril, Simi, Darey, Phyno, Seyi Shay na wengine.
Chini ni orodha ya washindi kwenye tuzo hizo pamoja na picha za ndani ya ukumbi na red carpet:
Artist of the Year
Wizkid
Song of The Year
Utanipenda – Diamond
Album of the Year
Ahmed Soultan
Revelation of the year
Falz
Video of the Year
Dogo Yaro – Vvip
Best African Collaboration
Eddy Kenzo ft Niniola – Mbilo Mbilo (Remix)
Best African Group
VVip
Best African Jazz
Jimmy Dludlu
Best Artist/Duo/Song Of The Year
Diamond – Utanipenda
Best Artist/Duo/Group in African Rock
Mvula
Best Artist/Duo/Group African Ragga & Dancehall
Patoranking
Best Artist/Duo/Group African RnB
Henok and Mehari Brothers
Best Artist/Duo/Group African Hiphop
Stanley Enow
Favourites Award
Phyno
Song writer of the year
Unique Muziki – Uganda
Most Promising Artiste
AmineAub
Artiste/Dou/GroupBand in African Contemporary
Flavour
Best female Artiste in Inspirational music
Naomi Achu
Best Male Artiste Western Africa
Flavour
Best female artiste Western Africa
Aramide
Best male artiste Northern Africa
Dj Van
Best male artiste S/Africa
BlackCoffee
Best female artiste S/Africa
Bruna Tatiana
Best Male Artiste Eastern Africa
Diamond Platnumz
Best Female Eastern Africa
Cindy Sanyu













Mwanamuziki mkongwe wa Cameron, Manu Dibango alitunukiwa pia tuzo ya heshima


Diamond na meneja wake, Sallam



Katikati ni Cindy Sanyu na Unique Music kutoka Uganda ambao wote walishinda tuzo

Mwanamuziki wa Nigeria, Seyi Shay

Kundi la Ghana, VVIP

Eddy Kenzo wa Uganda akishukuru baada ya kushinda tuzo

Rapper wa Nigeria, Falz naye aliibuka mshindi


Falz ni miongoni mwa wasanii walioshangiliwa sana wakati wa kutumbuiza

Ahmed Soultan alishinda album ya mwaka. Alikuwa MC pia kwenye show hiyo

Patoranking

Peter Okoye wa P-Square akitumbuiza na mwenzake kwenye show ya kufungia sherehe za tuzo hizo

Paul Okoye






Bonang Matheba akihojiwa kwenye red carpet

Bonang ambaye ni girlfriend wa AKA, alikuwa mmoja wa washereheshaji wa tuzo za Afrima 2016

Victora Kimani wa Kenya





Avril kutoka Kenya









↧
↧
Jokate amuandikia Alikiba barua kutoka kwenye sakafu ya moyo wake
Super business woman, Jokate Mwegelo amemuandikia AliKiba ujumbe mzuri ambao amedai umetoka kwenye sakafu ya moyo wake.

Mwanamitindo huyo ambaye yupo karibu zaidi na mkali huyo wa wimbo ‘Aje’ amemsifia msanii huyo huku akiichambua show yake aliyoifanya usiku wa kuamkia Jumapili katika tamasha la Fiesta Dar es salaam.
Kupitia Instagram, Jokate ameandika:
Komando Kipensi @officialalikiba kwanza thank you for trusting me and @noelgiotz to style you for Fiesta- tulielewa how important this day is to you and I’m glad we made it . It was fun creating this iconic look, you made it easy though I mean your body is just perfect and the way you carry yourself with so much class and honor you just gave this outfit the life and sophistication it needed. Style yako ya mavazi ni ya kipekee, hugezi mtu unatengeneza yako kama unavyofanya na mziki wako, ni halisi. Sasa mimi napenda kuongea nikiguswa, sio kama AK ila baada ya kuona ulichofanya jana kwenye stage ya fiesta ( umeimba live na band kwenye umati mkubwa vile kwa ustadi mkubwa kabisa mpaka watu wakashtuka maana you were simply perfect ) naomba kusema tu wewe hushindani na yoyote hapa Tanzania, kuanzia ladha yako ya mziki unaotengeneza mpaka sauti yako – tena huko kwenye sauti naomba nisiongee maana sitaki upasuke bichwa lako lol ila kuna kitu cha kipekee kwenye sauti yako, you are “The Voice”. Kila siku unakuwa bora zaidi yaani labda nikufananishe na Beyonce kimziki- usiniue lakini . Ukitaka you can dance, you can sing tena live sauti cleeeear haina mikwaruzo, you can rap, unaeeza igiza uchizi yaani you are just perfect kama mwanamuziki. Kama hujui leo ujue. Nakuombea siku mmoja dunia nzima iweze kufurahia hiki kipaji adhimu kutoka kwako. Unajua kuna tofauti ya kuimba wimbo au kusikiliza wimbo tu kama burudani na kusikiliza kitu kinachokuinua spiritually. Kitu kinagusa roho yako. Nikisikia Aje, Mwana, My Everything, Mali yangu hata kama nina mood mbaya vipi my soul becomes happy yaani naturally. You are a gem na utafika tu. Huu mwendo wako huu huu ndio poa. Wasikuchanganye. Nikiangalia mfano wa Wizkid yeye anafanya mziki wake, focus yake niyeye na fans wake na ndio maana yuko alipo licha ya kushindanishwa na watu kutwa nzima. Blood fans wa AK najua mko nae tumlazimishe huyu kijana afanye tour nchi nzima pekee yake labda . Haya mambo ni makubwa wallahy. All in all I’m very proud of you na your journey of growth and WTH man start giving me credit on the lyrics I help you with . Hongera @cloudsfmtz kwa show nzuri na kwa wasanii wote #Kajiandae #KingKiba #Kidoti
↧
Lowassa Atikisa Bunge Kwa Mara Nyingine
Edward Lowassa bado angali vinywani mwa wabunge japokuwa hayupo tena Bungeni .Jina lake jana limeibua mjadala bungeni wakati wabunge walipotoleana maneno makali kuhusu waziri huyo mkuu wa zamani.
Sakata hilo limetokea wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipokuwa likijadili Muswada wa Huduma ya Habari ambao ulipitishwa jana licha ya kupingwa vikali na kambi ya upinzani na wadau wa habari.
Lowassa amelizua tafrani bungeni baada ya wabunge wawili kurushiana maneno kuhusu taarifa zake tofauti zilizokuwa zikiandikwa na vyombo vya habari kiasi cha kusababisha mwenyekiti wa Bunge aingilie kati.
Akichangia muswada huo, mbunge wa viti maalumu (CCM), Amina Mollel amerejea sakata la zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo ilibainika baadaye kuwa haikuwa na uwezo. Sakata hilo lilitokea wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu.
“Mimi naomba ninukuu baadhi ya vichwa vya habari ambavyo vilitumiwa katika magazeti,” amesema Mollel, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.
Mollel ametaja mfano wa gazeti lililoandika “Lowassa anajua uzalendo au ni machozi ya mamba” na kichwa kingine cha habari cha gazeti hilo kilichosema “Lowassa Hasafishiki” na kingine kilichosema “Lowassa karibu Chadema”.
“Kuna haja ya kuwa na waandishi ambao leo hii wanaandika habari kwamba mtu huyo ni mbaya lakini kesho hiyo hiyo uongo huo unabadilika na kuwa ukweli?”amehoji Mollel.
Amesema Taifa linahitaji kuwa na sheria kama hiyo ambayo inaweza kulinda taaluma ya waandishi wa habari, hivyo kupitishwa muswada huo ni kwa manufaa ya wanahabari.
Maneno hayo kuhusu Lowassa yakamfanya mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji kusimama na kutumia methali inayosema “ukienda kwa wenye chongo, ufumbe macho ili ufanane nao japokuwa unaona”.
“Leo kituko cha karne hii ni pale anaponyanyuka mbunge wa CCM ndani ya Bunge akatulaumu eti sisi (wabunge wa kambi ya upinzani) kwa sababu tunampenda Lowassa. Hiki ni kituko cha karne,” amesema.
“Rudini kwenye kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa CCM kuhusu kale kawimbo katamu. Kweli?” amesema na kufanya wabunge wengine wa upinzani kuanza na kuimba “tuna imani na Lowassa”.
Jina la Lowassa limekuwa likiibuka kwenye vikao mbalimbali na katikati ya mwaka lilikuwa gumzo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ulioitishwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho,
↧
Fiesta 2016 Imooo Yatikisa Jiji la Dar
Mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade akizikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria tamasha la Fiesta 2016 Imoooo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

Mwanamuziki kutoka Nigeria, Tekno Miles akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016.
Mashabiki wakifuatilia shoo ya Fiesta 2016 ndani ya Viwanja vya Leaders Club usiku huu.
Tekno na vijana wake wakifanya yao.
Ali Kiba “King Kiba” akiwapa raha mashabiki wake waliofurika katika Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya Fiesta 2016.

King Kiba akiimba sambamba na King of the best melodies, Christian Bella.
King Kiba akizidi kuwapa raha mashabiki.

Baraka Da Prince akikatika sambamba na madansa wakati akiimba wimbo aliomshirikisha Ali Kiba.
Abby Skillz akiimba jukwaani wimbo aliomshirikisha Kiba.
Mwana Hip hop, Roma Mkatoliki akishusha mistari juu ya jukwaa la Fiesta 2016.
Roma Mkatoliki na Stamina wakiwa stejini na mavazi yao ya mabondia.
Chid Benz akifanya yake.
Mr Blue akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika hitimisho la msimu wa Fiesta 2016.
Mwanamuziki Chegge Chigunda na madansa wake wakionyesha umahiri wao stejini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media ambao ni waandaaji wa Fiesta wakiwa stejini.
Mwanamuziki Ben Pol akiwaburudisha mashabiki.

Mwana RnB, Ben Pol akiwapa raha mashabiki.
Mashabiki wakiwa wakolea na burudani za Fiesta 2016.

Burudani zikiendelea.
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akisema na mashabiki.
Dogo Janja akikisanua stejini.
Mzee wa Too Much, Darasa akiwapa shangwe wapenda burudani.
Mwanamuziki TID a.k.a Mnyama a.ka. Kigoo akifanya yake kwa steji.
King of the best melodies, Christian Bella akiwapa raha Wana Dar es Salaam.
Mwanamuziki Raymond “Rayvan” kutoka WCB akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016 Imooo.
Nyomi ikifuatilia shangwe za Fiesta 2016 Imooo.
Vijana wakionyesha umahiri wao wa kucheza ‘karate’.
Hatimaye ile shoo kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa burudani jijini Dar es Salaam ili kuhitimisha msimu wa Fiesta 2016 imefanyika leo Novemba 5, 2016 ndani ya Viwanja vya Leaders Club na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo.
Shoo hiyo imeongozwa na wasanii kutoka nje ya nchi wakiwemo Tekno Miles “Tekno” na Yemi Alade wote kutoka Nigeria pamoja na Dk. Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.
Wasanii wa hapa waliozikonga nyoyo za mashabiki wa burudani ni pamoja na Alikiba “King Kiba”, Weusi, Juma Nature, Mr Blue, Darasa, Christian Bella “King of the best melodies”, J Mo, Jux, Shilole, Snura, Raymond “Rayvan”, Baraka Da Prince, Vanessa Mdee, TID, Roma Mkatoliki, Stamina, Fid Q, Ommy Dimpoz, Abby Skillz, Dogo Janja, Billnas, Young D, Belle 9, Barnaba na wengineo.
↧
Video: Mahakama Yaamuru Jide Awaombe Radhi Viongozi wa Clouds

DAR ES SALAAM: Mahakama ya Wilaya Kinondoni leo Jumatano, Novemba 2, 2016, imemtia hatiani mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo “Lady Jaydee” (pichani juu) kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya viongozi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.
Mahakama hiyo imemuamuru aombe radhi kupitia kwenye chombo cha habari chenye “coverage” kubwa nchini kote na ikiwezekana duniani.

Joseph Kusaga.
Katika kesi hiyo, Jaydee anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti wa Redio hiyo, Ruge Mutahaba kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Ruge Mutahaba.
Mei 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jaydee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kesi inayomkabili msanii Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee dhidi ya walalamikaji Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kesi namba 29 ya Mwaka 2013 hukumu yake imetolewa leo na Hakimu wa mahakama ya Wilaya Boniphace Lihamwike kuwa wameridhishwa na ushahidi uliotolewa kuwa msanii huyo alitenda kosa la kuwadhalilisha na kuwakebehi kwa maneno machafu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ndugu Ruge Mutahaba.
Hhivyo Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeamuamuru msanii huyo kuomba radhi katika chombo cha habari cha kitaifa au kinachosikika kimataifa pamoja na duniani nzima kuwa maneno yake yalikuwa ya kashfa na udhalilishaji yenye lengo la kuichafua taswira nzuri ya ndugu Kusaga pamoja na ndugu Ruge Mutahaba vilevile Mahakama imemuamuru Jide msanii huyo kulipa fidia na gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo.
Hukumu ya kesi hiyo iliyosomwa leo saa 2:30 asubuhi katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni upande wa Msanii Judith Wambura uliwakilishwa na Wakili wake aitwaye Advocate Chacha licha ya msanii huyo kuhudhuria mahakamani hapo na kushindwa kushuka kwenye gari aina ya Noah waliyokuwa wamefika nayo Mahakamani hapo akiambatana na Meneja wake Seven Mosha ambaye alizuiliwa getini na walinzi kutokana na kuvaa nguo isiyozingatia maadili ya Mahakama.
Mwenendo wa kesi hiyo iliyofunguliwa tangu mwaka 2013 kwa msanii huyo akituhumiwa kuwatukana, kuwakebehi pamoja na kuwakashifu ndugu Joseph Kusaga pamoja na Ruge Mutahaba kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano aliyokuwa akifanya mara kwa mara na vyombo tofauti vya habari.
Tangu kesi hiyo ilipofunguliwa msanii huyo amekuwa na mwenendo usiokuwa wa kuridhisha na kumfanya kushindwa kesi hiyo ni pamoja na;
1. Kukosa ushahidi wa yale aliyokuwa akiyazungumza yeye binafsi kwamba ametendewa na kufanyiwa na washtaki,
2. Kukosa mashahidi wa kusimama mahakamani kutetea alichokuwa anakisema kwani mpaka kesi inamalizika hakuweza kuleta shahidi hata mmoja. upande wa washitaki uliweza kuleta mashahidi takribani 15 mpaka hukumu ya kesi inasomwa hii Leo.
3. Kutokuhudhuria mahakamani yeye mwenyewe, jambo linalotafsiriwa na wengi kama kutokuwa makini lakini pia kukurupuka kwa yale aliyokuwa akiyasema na kuandika kwani inawezekana kabisa sababu tajwa hapo juu zilimfanya aingie mitini.
Moja kati ya maneno yaliyomtia hatiani Jaydee ni wosia aliouandika May 2013 kupitia blog yake.
Wosia huo ulisomeka:
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye
maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi. Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari. Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa. Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria. Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia. Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa. Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao. Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu. Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu. Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu. Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka. Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu. Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili. Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi?? Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili. Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu. Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo?? Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu.
Licha ya hukumu hiyo kutolewa, Meneja wake, Seven Mosha, amesema kuwa Lady Jaydee atatoa maelezo yake kuhusu hukumu hiyo muda si mrefu
↧
↧
Wizkid Ambwaga Alikiba, Ashinda MTV Ema Award
↧
Wema Sepetu 'Me I dont Deal With Washamba, Nilijua Muna Alikuwa Mshamba Alivyokuja ila Nikaweka Ustaa Pembeni na Kumkubali'
Wema Sepetu Akihojiwa na Kipindi cha E News cha Clouds FM ameulizwa kuhusu beef lake na Muna na Kudai kuwa yeye huwa hadeal na Washamba akaongeza kusema kuwa urafiki na Muna ulikuja na kuuruhusu akijua Muna ni Mshamba lakini alikubali kuweka Ustaa Wake pembeni na kukubali awe Rafiki yake lakini mwisho wake ndio yaliyotokea....
'Me I dont deal with washamba, i knew she was mshamba alivyokuja lakini nilisema nisiweke ustaa nimchukulie kama vile jinsi alivyo'
'Me I dont deal with washamba, i knew she was mshamba alivyokuja lakini nilisema nisiweke ustaa nimchukulie kama vile jinsi alivyo'
↧
Sakata la Diva Kudai Jokate ni Gundu Kwa Ali Kiba..Gigy Money Afunguka Haya
Mwanadada Diva aliweza ku tweet kuhusiana na uwezo wa alikiba katika kuimba na kumalizia kuwa “Girlfriend anakutia gundu” kitu ambacho wengi walijiuliza inamaana Jokate (Kama inavyo julikana kuwa ndiye wa Kiba) kuwa anamtia gundu?
Leo Mrembo Gigy_Money amejitokeaza na kupost picha hii hapa chini na kuandika maneno ya kumtetea Jokate:
"Honestly jojo wangu mtoto classic uyu 😍wache waseme unagundu ila mwisho wa siku watakuelewa tu kwa mafanikio yako hadi unafikia umri wao yani we utakua Michael Jackson wa kike unajituma mwaya #USIFORCETUFANANE #HATUFANANI" Gigy Money
↧
Hii ni kauli ya mwisho ya Sitta baada ya kuambiwa na daktari hawezi kupona
Mtoto wa marehemu Samweli Sitta,ambaye pia ni Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta amesema kabla ya kifo cha mzee sita alisema “that is life (hayo ndiyo maisha) baada ya kuambiwa na daktari kwamba ugonjwa unaomsumbua hawezi kupona.
![]()
Benjamini amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kilichopelekea kifo cha baba yake kutokea alieleza kuwa baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume.
“Ni mzee ambaye tunampenda sana ni mzee ambaye ni baba sio tu kwa familia ya Mzee Sitta lakini ni baba kwa watu wengi, kwa masikitiko makubwa tumempoteza baba yetu kipenzi ambaye alisumbuliwa na Saratani ya tezi dume ambayo ilipozidi ilianza kushambulia viungo vingine na mguu akawa anapata shida kutembea,lakini yote mipango ya Mungu alitutoka mida hiyo ya saa saba na nusu Ujerumani ikiwa ni saa tisa na nusu alfajiri,”alisema Benjamin.
“Sasa mipango mingine inapangwa na Bunge pamoja na serikali wao ndiyo wahusika sasa hivi kwasababu ni kiongozi kitaifa lakini zaidi ya hapo naamini ndani ya hizo siku mbili tatu mwili utakuwa umekuja na watu watapata fursa ya kumuaga lakini kutakuwa na kwenda kumzika Urambo ambako naamini ndio nchi yake yeye kule ndiko aliko anzia na anakwenda kumalizia kule kwahiyo tuko kwenye majonzi nadhani taarifa na ratiba serikali Ikulu watatoa na maelekezo zaidi,”ameongeza.
BY : EMMY MWAIPOPO

Benjamini amezungumza hayo alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kutaka kujua kilichopelekea kifo cha baba yake kutokea alieleza kuwa baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume.
“Ni mzee ambaye tunampenda sana ni mzee ambaye ni baba sio tu kwa familia ya Mzee Sitta lakini ni baba kwa watu wengi, kwa masikitiko makubwa tumempoteza baba yetu kipenzi ambaye alisumbuliwa na Saratani ya tezi dume ambayo ilipozidi ilianza kushambulia viungo vingine na mguu akawa anapata shida kutembea,lakini yote mipango ya Mungu alitutoka mida hiyo ya saa saba na nusu Ujerumani ikiwa ni saa tisa na nusu alfajiri,”alisema Benjamin.
“Sasa mipango mingine inapangwa na Bunge pamoja na serikali wao ndiyo wahusika sasa hivi kwasababu ni kiongozi kitaifa lakini zaidi ya hapo naamini ndani ya hizo siku mbili tatu mwili utakuwa umekuja na watu watapata fursa ya kumuaga lakini kutakuwa na kwenda kumzika Urambo ambako naamini ndio nchi yake yeye kule ndiko aliko anzia na anakwenda kumalizia kule kwahiyo tuko kwenye majonzi nadhani taarifa na ratiba serikali Ikulu watatoa na maelekezo zaidi,”ameongeza.
BY : EMMY MWAIPOPO
↧
↧
Serikali Yaitaka sekta binafsi kuwekeza katika kinywaji aina Gongo ili kurasimisha kinywaji hicho

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezishauri kampuni zinazotengeneza vilevi kutengeneza pombe yenye ladha ya gongo, kwa kuwa baadhi ya wateja wanavutiwa na ladha hiyo wana wanakipenda kinywaji hicho.
Mwijage ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) aliyehoji mpango wa serikali wa kuanzisha na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya gongo ili kuchochea uchumi wa nchi na kubainisha kuwa, gongo ikitengenezwa kiwandani itafuata ubora unaotakiwa kisheria.
“Moja ya kigezo muhimu cha kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko, kutokana na wananchi kupenda kinywaji hiki(gongo) nawashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na ofisi za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa viwanda bora na salama vya aina hii,” alisema Mwijage.
Amesema haiwezekani Serikali kuhalalisha gongo, ila inaishauri sekta binafsi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi zinazotengeneza kinywaji hicho kwa lengo la kuzalisha kinywaji kinachokidhi viwango vya usalama na ubora wa chakula.
Katika swali la nyongeza, Masaba amehoji kama serikali ipo tayari kufanya utafiti kujua faida zilizo kwenye gongo.
Mwijage amesema faida zinafahamika, lakini atawaelekeza wataalamu wake waendele maeneo yenye gongo na pombe nyingine za kienyeji ili kuzifanyia utafiti na zitengenezwe kwa kufuata ubora na viwango.
↧
Wabunge waridhia msimamo wa Serikali wa kutokusaini mkataba wa EPA
↧
Etihad yazindua safari za Johnnesburg kwa kutumia ndege ya kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner

Shirika la Ndege la Etihad kupitia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner limeanzisha safari zake mpya katika Jiji la Johnnesburg kuanzia tarehe 01 Novemba 2016 mchana kwa uzinduzi wa ndege hiyo kutoka Abu Dhabi.
Ndege hiyo iliondoka Abu Dhabi saa 4:15 asubuhi na ilitarajiwa kuwasili saa 10:45 jioni. Pia ilitarajiwa kuondoka Jonhnnesburg 1:50 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa 12: 10 asubuhi kesho yake.
Ndege hiyo ya kisasa ya Etihad inayotoa huduma kwa madaraja ya kwanza na kawaida inatarajiwa kutoa huduma za kila siku katika jiji hilo…Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Uamuzi wa kutumia ndege hiyo ya kisasa zaidi kwa safari za Johnnesburg umelenga kukidhi mahitaji halisi ya wateja kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji huduma za daraja la kwanza na huduma bora kwa wanaokwenda na kutoka nchini Afrika Kusini.
Wasafiri wanaokwenda na wakati wanahitaji huduma nzuri, zenye ubunifu na salama, na matarajio yetu ni kutoa huduma zenye kiwango cha juu cha ubora zinazokidhi ukarimu na teknolojia ya hali ya juu ili kuifanya safari yako iwe ya kukumbukwa.”
Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Etihad nchini Afrika Kusini aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa ndege ya Boeing 787 kutaongeza maendeleo kwa kuvutia wageni wengi kutumia safari hizo. Ndege hii yenye ubora wa hali ya juu ina kila huduma ndani yake na mandhari ya kuvutia.”
Ndege hiyo ya kisasa imeundwa ikiwa na vitu mbalimbali ndani yake vitakavyokufanya uburudike na kusafiri kwa uhuru zaidi. Kuna vituo takriban 28 kwa daraja la kwanza na kuna vituo vyenye ubora 271 kwa ajili ya daraja la kawaida.
Kwa daraja la kwanza kuna huduma ya vitanda vyenye ukubwa wa kutosha na nafasi ya kutosha ya mtu kuburudika. Kuna vitambaa laini na vyenye kuvutia ambavyo vimezungushiwa kwenye kila kiti. Huku kukiwa na mfumo wa kielektroniki unaomwezesha mteja kusogeza kiti kwa kiwango anachotaka jambo linalompa uhuru zaidi akiwa safarini.
Kila chumba kwenye daraja la kwanza kuna runinga kubwa ya flat screen unayoweza kutumia kwa njia ya kugusa huku ukipata huduma ya vifaa vya kudhibiti kiwango cha kelele,
Vilevle hata kwenye daraja la kawaida kila kiti kina runinga ndogo pamoja na vifaa vya kusikilizia redio kwa wateja wanapokuwa safarini. Pia kuna viti vikubwa ambavyo vinamfanya mteja kuwa huru kuweka miguu kwa kadri anavyotaka.
Aidha kuna mfumo unaowawezesha wateja kutumia intaneti bure huku kukiwa na mahali ambapo abiria anaweza kuchomeka USB yake ili kuchaji simu na huduma zingine za kimawasiliano. Muda wote unapokuwa kwenye ndege hiyo utaburudika kwa kupata chaneli mbalimbali ambazo zinaonekana katika ubora wa hali ya juu huku wahudumu wakitoa huduma zilizotukuka kwa wateja.
Wahudumu wa ndege waliopo ni wabobezi kutoka vyuo vikubwa vinavyotambulika ulimwenguni kama vile Flying Nannies waliopata mafunzo Norland College nchini Uingereza kuhusuna na malezi ya watoto wanapokuwa kwenye ndege.
Pia kuna wasimamizi wa vyakula waliobobea ambao wamefanya kazi katika hoteli kubwa na maarufu duniani huku wakiwa na mafunzo ya kuhudumia daraja la kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa na ujuzi wa kuandaa vinywaji laini.
Wateja wanaotumia ndege hiyo watapata fursa ya kufurahia kuona mandhari ya nje kupitia madirisha makubwa na uwapo wa hali ya hewa tulivu.
Shirika la ndege la Etihad limekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wasafiri wake wanaotoka Afrika wanapofika kwenye mamlaka ya forodha nchini Marekani na Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi kukamilisha utaratibu wa wahamiaji kwa haraka.
Utaratibu huu ukiacha Shirika la Ndege la Etihad ukanda wa ghuba, inawapa fursa wateja kukamilisha taratibu zote muhimu za uhamiaji, ushuru na forodha pamoja na kushughulikia vibali vya usalama kwa wasafiri wanapofanya safari kati ya Abu Dhabi na Marekani jambo linalowawezesha kupunguza mlolongo mrefu wanapowasili katika uwanja wa ndege wa Marekani.
Jiji la Johnnesburg ni mji wa tisa kuhudumiwa na ndege aina ya B757-9 Dreamliner. Ndege hiyo pia inatoa huduma katika miji ya Brisbane, Düsseldorf, Perth, Riyadh, Shanghai, Singapore, Washington DC and Zurich
Ratiba ya ndege ya Dreamliner kutoka Abu Dhabi – Johannesburg:
Ndege No. | eneo | Kuondoka | Eneo | Kuwasili | Kipindi |
EY604 | Abu Dhabi | 10:15am | Johannesburg | 4:45pm | Daily |
EY603 | Johannesburg | 7:50pm | Abu Dhabi | 6:10am (+1) | Daily |
Muda wa kuondoka umeorodheshwa kulingana na muda wa eneo husika.
Photo caption
Ndege ya Shirika la Etihad ya Boeing 787-9 ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa O.R Tambo jijini Johnnesburg.
Picha zaidi unaweza kuangalia kupitia mtandao huu:https://eyviscomms.box.com/s/pzcgsyymd6krzzyevyksbeay66331gi4
↧
Alikiba Ameshinda MTV Ema Kwa Kura Lakini ni Ukweli Hakustahili zaidi ya Wizkid!
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA.Naomba hapa nitumie nafasi hii kufafanua kilichotokea ili kuweza kuondoa huu utata.
Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi.
Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo. Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki.
Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.
Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid.
Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile.
Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache.
By Sele Mkonje
Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi.
Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo. Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki.
Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.
Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid.
Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile.
Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache.
By Sele Mkonje
↧
↧
Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo c ha Joseph Mungai
↧
Filamu ya Wema na Van Vicker ‘Day After Death’ kuzinduliwa Valentine’s Day
Baada ya kiu ya muda mrefu kwa mashabiki wa filamu wa Wema Sepetu hatimaye mwigizaji huyo amesema filamu yake na mwigizaji wa Nigeria, Van Vicker ‘Day After Death’ itazinduliwa Valentine’s Day.
![]()
Malkia huyo wa filamu ambaye amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu, amesema tayari filamu hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uzinduzi tu.
“Nina movie yangu mpya na Van Vicker inakuja na nitaifanyia uzinduzi Valentine’s Day kwa sababu ni movie ya mapenzi,” Wema aliiambia Clouds TV.
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya matamasha mbalimbali ya ‘Usiku wa Vigoma’ ambayo yanaambatana na uzinduzi wa bidhaa zake mpya.

Malkia huyo wa filamu ambaye amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu, amesema tayari filamu hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uzinduzi tu.
“Nina movie yangu mpya na Van Vicker inakuja na nitaifanyia uzinduzi Valentine’s Day kwa sababu ni movie ya mapenzi,” Wema aliiambia Clouds TV.
Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya matamasha mbalimbali ya ‘Usiku wa Vigoma’ ambayo yanaambatana na uzinduzi wa bidhaa zake mpya.
↧
Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Alfredo di Stefano
Mchezaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Alfredo di Stefano ya mchezaji bora wa La Liga msimu uliopita iliyotolewa na gazeti la Marca jana muda mfupi baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na Real Madrid.

Cristiano Ronaldo akiwa amebeba tuzo ya Alfredo di Stefano


Mchezaji mwingine wa Real Madrid Alvaro Morata nae ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Hispania wakati kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ameshinda tuzo ya Miguel Munoz ya kocha bora wa mwaka.

↧